• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango takwimu na Usuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Tehama
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uru kaskazini
    • Kata
      • Arusha chini
      • Kahe
      • Kahe mashariki
      • Kibosho kati
      • Kibosho kati
      • Kibosho magharibi
      • Kibosho mashariki
      • Kilema kaskazini
      • Kilema kati
      • Kilema kusini
      • Kimochi
      • Kindi
      • Kirima
      • Kirua vunjo kusini
      • Kirua vunjo magharibi
      • Kirua vunjo mashariki
      • Mbokomu
      • Mabogini
      • Makuyuni
      • Mamba kaskazini
      • Mamba kusini
      • Marangu magharibi
      • Marangu mashariki
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kusini
      • Njia panda
      • Okaoni
      • Old moshi magharibi
      • Old moshi mashariki
      • Uru kaskazini
      • Uru kusini
      • Uru mashariki
      • Uru shimbwe
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogondogo
  • Kituo cha Habari
    • Gallery

MKUU WA WILAYA YA MOSHI AKUTANA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

Posted on: June 3rd, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Godfrey Eliakimu Mnzava azungumza  na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwenye Mkutano ambapo pia alipokea Taarifa ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali iliyowasilishwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu Lucas Msele.

Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya alisema yafuatayo;

Aliyapongeza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali  kwa kazi nzuri wanazozifanya,

Aliwataka kuendelea kufanya kazi kwa kufuata Sheria na taratibu zinazoongoza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali

Aliwataka kila mmoja katika Shirika lake kulinda Usalama wa Nchi.

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni moja ya sekta muhimu inayochangia maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. Kwa mujibu wa Mwongozo wa Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wa Mwaka 2024 Mamlaka za Serikali za Mitaa zinawajibika kusimamia Mashirika yanayofanya kazi katika maeneo yao.

Wilaya  ya Moshi ina Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 70 yaliyosajiliwa. Mashirika hayo yanafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya masuala mtambuka ndani ya Jamii, kusaidia makundi yanayoishi katika mazingira hatarishi, kutoa vifaa vya elimu na afya, ujenzi na ukarabati wa miundombinu, utunzaji wa mazingira, uongezaji wa thamani wa bidhaa za kilimo, uhamasishaji na uundaji wa vikundi vya ujasiriamali, utoaji wa msaada wa kisheria, haki za binadamu na elimu ya uraia.


Mkutano Mkuu  wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali umeandaliwa kwa lengo la kutambua mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Aidha kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za mashirika na kubadilishana uzoefu na mbinu zinazoibuka katika utekelezaji. Mkutano huu utaongeza uelewa wa jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ndani ya jamii na pia utasaidia  kukumbushana majukumu na wajibu wa serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.


  Wilaya ya Moshi imeendelea kufanya uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kama  ifuatavyo:

1.Kuhakikisha kuwa Mashirika yamesajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 11 ya mwaka 2005 na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 na kutambuliwa kwa cheti na Katiba yake.

2.Kuimarisha mfumo wa kitaasisi wa ubadilishanaji wa tarifa kati ya Wizara yenye dhamana na Mashirika yasiyo ya kiserikali, Wizara, sekretarieti za Mikoa Mamlaka za Serikali za mitaa, Sekta binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuwezesha mchango wa Mashirika hayo kutambuliwa na Serikali.

3. Kuhakikisha Mashirika yanafanya kazi kwa mujibu wa nyaraka zao za usajili na si vinginevyo kama inavyoelekezwa na kifungu cha 30(2) cha sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002.

4.Kutoa taarifa kwa vyombo vya Usalama na Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali pale inapobaini vitendo /viashiria vya uwepo wa shughuli za shirika kuwa kinyume na sheria na kuzorotesha /kuhatarisha ulinzi /Ustawi  na usalama wa nchi.

5.Kuhakikisha kuwa shirika linalotekeleza mradi /wafua inayozidi fedha za kitanzania Shilingi Milioni ishirini (20,000,000) linawasilisha barua ya idhini kutoka kwa msajili kulingana kanuni ya Mashirika yasiyo ya kiserikali Namba 609 ya mwaka 2018 kifungu cha kanuni 13(b).

6. Kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa inazingatia vipaumbele vya maendeleo ya Taifa, inaleta tija kwa jamii na kutatua changamoto zinazolizunguka eneo la utekelezaji wa mradi.

7. Kufuatilia taarifa za utekelezaji na za ukaguzi za robo Mwaka na za Mwaka .

8. Kuendelea kuandaa taarifa za utekelezaji kuhusu utendaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kila robo Mwaka na kuiwasilisha katika ngazi husika za maamuzi.

9.Kuratibu kikao cha mwaka cha mkutano Mkuu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika uratibu wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwa ni pamoja na:

•Mashirika kuweza kutekeleza shughuli za miradi mbalimbali na kutatua changamoto za jamii pale ambapo serikali ilipungukiwa. Katika kipindi hiki jumla ya Mashirika 70 Yameweza kutekeleza miradi ya maendeleo   na kutatua changamoto za Wananchi

•Huduma za jamii zimeweza kufika maeneo mengi zaidi mfano Jumla ya Watoto 2350 wanaoishi Wilaya ya Moshi wamesaidiwa vifaa vya shule chakula na kuweza kuendelea na masomo.

•Kugundua na kusuluhisha migogoro mbalimbali iliyotokea baina ya Mashirika kwa kushirikiana na Wizara na Mashirika katika kipindi hiki tumeweza kufanya utatuzi wa mashirika 2 yaliyokuwa na mgogoro baina ya viongozi wa Shirika na Bodi, na shilika lingine walikuwa wanagombania wateja kati ya shilika moja na linguine.

• Ushiriki maadhimisho mbalimbali  umesaidia kuleta ufanisi mkubwa wa  uelewa na hamasa kwa jamii  kupitia kauli mbiu na hotuba zinazotolewa.

•Hata hivyo Halmashauri imeendelea kufanya ufuatiliaji kushauri na kuchukua hatua  za kukabiliana na changamoto hizo na nyingine kuziwasilisha kwenye ngazi husika.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI June 09, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI 29-01-2024 January 29, 2024
  • MATOKEO YA USAILI KWA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III NA NAFASI YA WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU II TAREHE 06.02.2024 February 06, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDUKA KWA NAFASI YA DEREVA II TAREHE 09.02.2024 February 09, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURU YA WILAYA YA MOSHI

    May 30, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MOSHI AKUTANA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

    June 03, 2025
  • MAMA SAMIA LEGAL AID COMPAIGN YAFIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

    January 30, 2025
  • MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI

    December 17, 2024
  • Tazama yote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • report za halmashauri

Viunganishi linganifu

  • Tovuti Kuu ya serekali
  • Tovutu ya serekali mtandao (eGA)
  • Tovuti ya Mkoa Kilimanjaro
  • Tovuti ya wizara ya tamisemi
  • Tovuti ya wizara ya fedha
  • Tovuti ya wizara ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Muelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji

    Sanduku la posta: P.o.Box 3003 Moshi

    Simu ya Mezani: Phone 2751865

    Mobile:

    Barua pepe: Email : ded@moshidc.go.tz or info@moshidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma
    • Sera ya faragha

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Haki zote Zimeifadhiwa.