• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango takwimu na Usuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Tehama
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uru kaskazini
    • Kata
      • Arusha chini
      • Kahe
      • Kahe mashariki
      • Kibosho kati
      • Kibosho kati
      • Kibosho magharibi
      • Kibosho mashariki
      • Kilema kaskazini
      • Kilema kati
      • Kilema kusini
      • Kimochi
      • Kindi
      • Kirima
      • Kirua vunjo kusini
      • Kirua vunjo magharibi
      • Kirua vunjo mashariki
      • Mbokomu
      • Mabogini
      • Makuyuni
      • Mamba kaskazini
      • Mamba kusini
      • Marangu magharibi
      • Marangu mashariki
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kusini
      • Njia panda
      • Okaoni
      • Old moshi magharibi
      • Old moshi mashariki
      • Uru kaskazini
      • Uru kusini
      • Uru mashariki
      • Uru shimbwe
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogondogo
  • Kituo cha Habari
    • Gallery

MKURUGENZI MTENDAJI AWAFUNDA WATENDAJI KATA NA VIJIJI UKUSANYAJI WA MAPATO

Posted on: October 18th, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Ndugu Shadrack Mhagama, ameongoza kikao kazi maalum kilichowahusisha Watendaji wa Kata na Vijiji kutoka maeneo yote ya wilaya, kwa lengo la kufanya tathmini ya hali ya ukusanyaji wa mapato na kujadili mikakati ya kuongeza ufanisi katika usimamizi wa fedha za umma.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhagama aliwataka watendaji kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu, uwazi na kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma. Alisisitiza kwamba jukumu la ukusanyaji wa mapato ni la msingi katika uendelevu wa shughuli za maendeleo ya wananchi.

“Nawasihi watendaji wote muwe waaminifu katika kukusanya mapato ya serikali. Fedha hizi ni za wananchi na zinapaswa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Ni jukumu letu kuhakikisha kila senti iliyokusanywa inaingia kwenye akaunti rasmi ya Halmashauri kwa wakati.” alisema Mhagama.

Aidha, Mhagama alitoa onya kali kwa watendaji wanaochelewesha kuwasilisha fedha zilizokusanywa au kutumia mapato kwa matumizi yasiyoruhusiwa, akibainisha kuwa hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume na maagizo hayo.

“Hakutakuwa na huruma kwa mtumishi yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha za serikali au kuchelewesha kuziwasilisha. Halmashauri haitasita kuchukua hatua kali, ikiwemo kuwasilisha suala hilo katika vyombo vya uchunguzi.” aliongeza Mhagama.

Katika kikao hicho, washiriki walipata fursa ya kujadili changamoto zinazokabili ukusanyaji wa mapato, ikiwemo elimu ya ujazaji wa taarifa za ukusanyaji wa mapato kwenye mfumo wa FASS, ucheleweshaji wa baadhi ya makusanyo kutoka vyanzo vya ndani, pamoja na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu wajibu wao wa kulipa kodi na ada.

Mmoja wa washiriki wa kikao hicho, Ndugu Seif Issa , Mtendaji wa Kijiji cha Sango, alisema kikao hicho kimekuwa muhimu kwani kimetoa mwongozo wa wazi juu ya namna bora ya kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa njia za kidijitali na kuongeza uwazi katika matumizi.

“Tumepata mwanga mkubwa kuhusu wajibu wetu katika ukusanyaji wa mapato. Kwa sasa tutaendelea kutumia mifumo ya kielektroniki kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wananchi wanaelimishwa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi,” alisema Seif.

Kwa upande wake, Ndugu Kamashaz Mhunga, Mtendaji wa Kijiji cha Kindi, alisema kuwa kikao hicho kimekuwa chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi wa watendaji vijijini.

“Mkurugenzi ametutia moyo lakini pia ametukumbusha wajibu wetu wa kisheria. Tunaenda kuhakikisha mapato yote yanaingizwa kwa wakati na matumizi yote yanafuata taratibu,” alisema.

Mkurugenzi Mhagama aliwaagiza watendaji wote kuweka mikakati ya ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato, hususan katika sekta za kilimo, mifugo na utalii wa ndani, huku akisisitiza kuwa Halmashauri ya Moshi itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.

“Tunataka kuona mapato yanaongezeka, huduma zinaboreshwa na wananchi wanapata maendeleo. Hiyo ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alihitimisha Mhagama

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa idara, wakiwemo Mkuu wa Idara ya Fedha, Mkuu wa Idara ya Rasilimani Watu na Utawala, Maafisa Habari, Wakaguzi wa Ndani pamoja na Wakuu wa Idara.

Matangazo

  • TANGAZO LA UTEUZI WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA NA KUITWA KWENYE MAFUNZO KWA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI NA VUNJO October 18, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI 29-01-2024 January 29, 2024
  • MATOKEO YA USAILI KWA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III NA NAFASI YA WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU II TAREHE 06.02.2024 February 06, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDUKA KWA NAFASI YA DEREVA II TAREHE 09.02.2024 February 09, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI MTENDAJI AWAFUNDA WATENDAJI KATA NA VIJIJI UKUSANYAJI WA MAPATO

    October 18, 2025
  • UTT AMIS YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

    October 07, 2025
  • WATAINIWA WA KIDATO CHA SITA 2025 MOSHI DC WAFAULU KWA ASILIMIA 100

    July 08, 2025
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2025 HALMASHAURU YA WILAYA YA MOSHI

    May 30, 2025
  • Tazama yote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • report za halmashauri

Viunganishi linganifu

  • Tovuti Kuu ya serekali
  • Tovutu ya serekali mtandao (eGA)
  • Tovuti ya Mkoa Kilimanjaro
  • Tovuti ya wizara ya tamisemi
  • Tovuti ya wizara ya fedha
  • Tovuti ya wizara ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Muelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji

    Sanduku la posta: P.o.Box 3003 Moshi

    Simu ya Mezani: Phone 2751865

    Mobile:

    Barua pepe: Email : ded@moshidc.go.tz or info@moshidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma
    • Sera ya faragha

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Haki zote Zimeifadhiwa.