• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango takwimu na Usuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Tehama
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uru kaskazini
    • Kata
      • Arusha chini
      • Kahe
      • Kahe mashariki
      • Kibosho kati
      • Kibosho kati
      • Kibosho magharibi
      • Kibosho mashariki
      • Kilema kaskazini
      • Kilema kati
      • Kilema kusini
      • Kimochi
      • Kindi
      • Kirima
      • Kirua vunjo kusini
      • Kirua vunjo magharibi
      • Kirua vunjo mashariki
      • Mbokomu
      • Mabogini
      • Makuyuni
      • Mamba kaskazini
      • Mamba kusini
      • Marangu magharibi
      • Marangu mashariki
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kusini
      • Njia panda
      • Okaoni
      • Old moshi magharibi
      • Old moshi mashariki
      • Uru kaskazini
      • Uru kusini
      • Uru mashariki
      • Uru shimbwe
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogondogo
  • Kituo cha Habari
    • Gallery

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI (ROBO YA KWANZA, JULAI – SEPTEMBA, 2023)

Wednesday 14th, May 2025
@Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Moshi

Afisa Lishe Wilaya Ndg. John Lwena awasilisha Taarifa ya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Kipindi cha Robo ya Kwanza Julai - Seotemba 2023 mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ndg.Kisare M. Makori ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao pamoja na wajumbe wengine kutoka Halmashauri.


Katika Taarifa yake Afisa Lishe alieleza yafuatayo;

Halmashauri ya Wilaya ya Moshi inaendelea kutekeleza afua mbalimbali za Lishe kwa kuzingatia viashiriavya Mkataba wa Lishe kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata na Vijiji, Wahudumuwa Afya ngazi ya Jamii na watoa Huduma za Afya vituoni, kwa lengo la kuboreshana kuimarisha afya na Lishe ya watoto, vijana balehe, wajawazito,wanaonyonyesha na wanawake waliopo katika umri wa kuzaa.

Katika kipindi cha robo ya kwanza (Julai-Septemba, 2023) Halmashauri imefanya jitihada kubwa katikautekelezaji wa afua za Lishe ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kiasi cha Tsh.26,635,831.99 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za Lishe. Kwa upande wa matumizi,Halmashauri imetumia jumla ya Tshs. 26,534,600.00 (99.6%) kutekeleza shughulimbalimbali za Lishe kwa robo ya kwanza. 

Matumizi ya fedha hizoyalielekezwa katika maeneo yafuatayo;

Usimamizi shirikishiwakati wa Maadhimisho ya Wiki ya unyonyeshaji Duniani, 

Vikao vya kamati ya Lishena tathimini ya mkataba wa Lishe, 

Ununuzi wa vibao 28 vyakupimia urefu kwa watoto wenye umri chini ya mitano, 

Utoaji wa nyongeza yamatone ya vitamini A kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya na Kuhamasishajamii juu ya matumizi ya mazao yaliyoongezwa virutubishi kibaolojia.

Taarifa hii inaangaziautekelezaji wa afua za Lishe katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wafedha 2023/24, kuanzia Julai hadi Septemba 2023. Aidha, taarifa hii imeanishamatumizi ya fedha na mchanganuo wake katika robo husika.

Katika kipindi cha Julai- Septemba, 2023, jumla ya Vijiji 153 kati ya 166 sawa na 92.2 % vimefanikishamaadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji.Maadhimisho hayo yalihusishashughuli mbali mbali za afya na Lishe kama vile upimaji wa hali ya Lishe kwawatoto wenye umri chini ya miaka 5 na kutoa elimu ya Lishe kwa jamii. 

Asilimia kubwa ya Vijijivilivyofanya maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji vinaonyeshamafanikio makubwa katika kuelimisha jamii kuhusu afya na Lishe bora.. 

Maadhimisho ya siku yaafya na Lishe ya kijiji ni chachu muhimu katika kuboresha afya na Lishe yajamii na ni muhimu kuendelea kuzipa kipaumbele katika mipango ya maendeleo yaVijiji na Halmashauri kwa ujumla. 

Pia shule za msingi nasekondari zimeendelea na zoezi la utoaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzishuleni na hii ni muhimu kwa afya bora, mahudhurio mazuri, kuongeza ufaulu nakupunguza utoro. Taarifa zilizokusanywa na Watendaji wa Kata zinaonyesha kuwajumla ya shule 367 (shule za msingi 266 na sekondari 101) sawa na asilimia 100zinatekeleza mpango wa chakula shuleni.

Utoaji wa elimu naunasihi wa ulishaji wa vyakula vya nyongeza imeendelea kutolewa kwa wazazi nawalezi wenye watoto walio na umri wa miezi 0 hadi 23 kupitia Wahudumu wa Afyangazi ya Jamii, kwenye maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji,mikusanyiko mbalimbali pamoja na kuwatembelea nyumba kwa nyumba na kupima haliya Lishe.

Katika kipindi chaJulai-Septemba,2023, jumla ya wazazi/walezi 6,272 (84.5%) kati ya 7,423wamepewa elimu na unasihi wa ulishaji wa watoto wadogo na wachanga kupitiaWahudumu wa Afya ngazi ya Jamii. 

Kanuni au sheria za Lisheni sera ambazo zinaweka mfumo wa kisheria wa kusimamia masuala ya chakula naLishe kwa jamii. Kanuni hizi zinalenga kuzuia utapiamlo na magonjwayanayosababishwa na Lishe duni. Kanuni na sheria za Lishe hujumuisha mambo kamavile miongozo ya lishe, usimamizi wa vyakula, usalama wa vyakula, na udhibitiwa Lishe duni.

Jumla ya Vijiji 157 vinakanuni na sheria za lishe zinatumika kuwachukulia hatua wazazi wazembe katikamasuala ya Lishe, malezi na makuzi ya watoto.

Katika kipindi chautekelezaji wa shughuli za Lishe (Julai-Septemba,2023), Halmashauri imepatamafanikio yafuatayo;

(i) Utoaji wa Elimu yaLishe: Halmashauri imeendelea kutoa elimu ya Lishe kupitia majukwaa mbalimbalikama vile Vyombo vya Habari, vituo vya kutolea huduma Pamoja na kupitiamaadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji.

• Halmashauri imefanikiwakufanya vipindi viwili vya elimu ya Lishe kuhusu mitindo bora ya Maisha nakuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama kwenyemaadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kupitia KR FM Redio.

• Elimu ya Lisheimeendelea kutolewa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na kwenyemaadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Vijiji kupitia Wahudumu wa Afya ngaziya Jamii. Elimu hiyo ililenga kuhamasisha ulaji unaofaa na mitindo bora ya maisha,umuhimu wa Lishe bora, unyonyeshaji, na unasihi wa ulishaji wa watoto wadogo nawachanga. 

(ii) Halmashauriimefanikiwa kununua vibao 20 vya kupimia udumavu na kuvisambaza kwenye vituovya kutolea Huduma za Afya kwa ajili ya kufuatilia hali ya udumavu kwa watotowenye umri chini ya miaka 5.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI May 12, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI 29-01-2024 January 29, 2024
  • MATOKEO YA USAILI KWA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III NA NAFASI YA WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU II TAREHE 06.02.2024 February 06, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDUKA KWA NAFASI YA DEREVA II TAREHE 09.02.2024 February 09, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MAMA SAMIA LEGAL AID COMPAIGN YAFIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

    January 30, 2025
  • MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI

    December 17, 2024
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA VUNJO NA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU 2 KWA MAAFISA WATENDAJI WASAIDIZI NGAZI YA KATA YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    December 04, 2024
  • UANDIKISHAJI WA WAPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

    October 11, 2024
  • Tazama yote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • report za halmashauri

Viunganishi linganifu

  • Tovuti Kuu ya serekali
  • Tovutu ya serekali mtandao (eGA)
  • Tovuti ya Mkoa Kilimanjaro
  • Tovuti ya wizara ya tamisemi
  • Tovuti ya wizara ya fedha
  • Tovuti ya wizara ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Muelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Moshi District Council

    Sanduku la posta: P.o.Box 3003 Moshi

    Simu ya Mezani: Phone 2751865

    Mobile:

    Barua pepe: Email : ded@moshidc.go.tz or info@moshidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma
    • Sera ya faragha

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Haki zote Zimeifadhiwa.