• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango takwimu na Usuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Tehama
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uru kaskazini
    • Kata
      • Arusha chini
      • Kahe
      • Kahe mashariki
      • Kibosho kati
      • Kibosho kati
      • Kibosho magharibi
      • Kibosho mashariki
      • Kilema kaskazini
      • Kilema kati
      • Kilema kusini
      • Kimochi
      • Kindi
      • Kirima
      • Kirua vunjo kusini
      • Kirua vunjo magharibi
      • Kirua vunjo mashariki
      • Mbokomu
      • Mabogini
      • Makuyuni
      • Mamba kaskazini
      • Mamba kusini
      • Marangu magharibi
      • Marangu mashariki
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kaskazini
      • Mwika kusini
      • Njia panda
      • Okaoni
      • Old moshi magharibi
      • Old moshi mashariki
      • Uru kaskazini
      • Uru kusini
      • Uru mashariki
      • Uru shimbwe
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogondogo
  • Kituo cha Habari
    • Gallery

Epuka maambukizi mapya ya VVU

Posted on: December 1st, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imeungana na taasisi zingine za serikali na zisizo za serikali katika kuazimisha siku ya UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) duniani leo tarehe 01 Desemba 2018. Maazimisho hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Mwika iliyopo kata ya Mwika Kaskazini , kijiji cha Maring’a ndani ya Wilaya ya Moshi.


Tukio hilo limehudhuriwa na wanafunzi wa Mwika,wataalam mbalimbali,wadau wa masuala ya kupambana na ugonjwa wa UKIMWI na mamia ya wananchi wa kata ya Mwika.Kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka 2018 ni “Pima ,Jitambue,Ishi”. UKIMWI husababishwa na  Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Sherehe hizo zimepambwa na shamrashamra nyingi  ikiwemo maigizo,ushairi,nyimbo na makala. Shamrashamra hizo zimesheheni elimu, jumbe nzito,makatazo na maonyo makali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu ugonjwa hatari wa UKIMWI.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Peter Malendecha ambae ndiye mgeni rasmi katika tukio hili ameitaka jamii kuhamasika katika suala la kupima na kutambua afya zao kwani ni muhimu na faida kwao kwa kuwa unapojitambua mapema inakupa fursa ya kuanza dawa mapema na kuweka mipango ya maisha yako vizuri zaidi.

Mhe. Malendecha ametoa takwimu za kitaifa zinazoonyesha kuwa ni asilimia 52.2 tu ya wananchi wenye umri  wa miaka 15 hadi 64 ndiyo wanaojua hali zao ikilinganishwa na lengo la kitaifa la asilimia 90 lililowekwa ifikapo mwaka 2020.

Sambamba na hayo Mhe.Malendecha ameiasa na kuitaka jamii ya Moshi kwa ujumla kujikinga na maambukizi mapya,kuacha kufanya ngono zembe,kwa walioathirika kuendelea kutumia dawa kwa ufasaha ili kupunguza kasi ya virusi kuzaliana mwilini pamoja na kina mama wajawazito kupima na wenza wao wakati wa kuhudhuria kliniki ya wajawazito.

Wakati wa maadhimisho hayo mada zinahusu jamii na UKIMWI ziliwasilishwa na wataalam wa Maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.

Afisa maendeleo ya jamii Bi Bertha Yairo amewaasa jamii ya Moshi kwa ujumla juu ya masuala ya ukatili unaofanyika katika jamii huku wahusika na waathirika wake wakubwa wakiwa ni kina mama na watoto. Amezitaka jamii kuacha mara moja vitendo hivyo vya ukatili kwani ni kinyume cha haki za binadamu.

Bi Yairo ameongeza kuwa zipo aina nyingi za ukatili ambao huchangia katika maambukizi ya VVU kama vile ukatili wa kijinsia ,kingono,kulawitiwa na ukeketaji.Hivyo ni jukumu la jamii kutokaa kimya.”Jamii ya Moshi tupaze sauti juu ya majanga ya ukatili wa aina yoyote ,tuokoe kizazi chetu”amesema .

Bi.Yairo ameweka wazi kuwa waathirika wa ukatili wanaweza kutoa taarifa maeneo mbalimbali kama vile ngazi ya familia majumbani,ofisi ya Mtendaji wa kijiji,ofisi ya Mtendaji wa kata,Afisa Ustawi wa jamii aliyepo jirani , polisi .

Aidha Mratibu wa UKIMWI ngazi ya Wilaya Bi.Lydia Njau ameijulisha jamii uwepo wa mpango taifa wa serikali juu ya asilimia 90 tatu,ambapo 90% ya kwanza inamaanisha kufikia mwaka 2020 tunapaswa kufikia 90% ya watu kujua hali zao za maambukizi ya VVU,90% ya pili inamaanisha watakaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU wawe kwenye dawa za kufubaza VVU na 90% ya tatu ikimaanisha wanaotumia dawa kuwa na VVU vilivyofubazwa.

Mhe.Malendecha amehitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi wote wa Wilaya ya Moshi kupima, ’’WanaMoshi hasahasa wanaume tujitokeze kwa wingi katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya ,tupime kujua afya zetu,kwa wale watakaogundulika kuwa na maambukizi waanze dawa za kufubaza VVU mara moja.Tutekeleze kauli mbiu yetu ya Pima,Jitambue,Ishi”  .

Matangazo

  • Kuhama kwa ofisi za makao makuu ya Halmashauri November 05, 2019
  • Ujio wa wageni kutoka Ujerumani October 29, 2019
  • TANGAZO LA KAZI May 22, 2019
  • Umezeshaji kinga tiba kwa watoto April 26, 2019
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • "Tuwajibike kwa kiwango cha kutosha katika nafasi zetu"- Mhe. Kippi

    November 12, 2019
  • Uzinduzi wa kitalu cha miti Himo

    October 30, 2019
  • Karibu wageni kutoka Kiel

    October 29, 2019
  • "Maziwa,chakula na pesa"-Mama Mghwira

    October 23, 2019
  • Tazama yote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • report za halmashauri

Viunganishi linganifu

  • Tovuti Kuu ya serekali
  • Tovutu ya serekali mtandao (eGA)
  • Tovuti ya Mkoa Kilimanjaro
  • Tovuti ya wizara ya tamisemi
  • Tovuti ya wizara ya fedha
  • Tovuti ya wizara ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Muelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Moshi District Council

    Sanduku la posta: P.o.box 3003 Moshi

    Simu ya Mezani: Phone 2751865

    Mobile:

    Barua pepe: Email : info@moshidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma
    • Sera ya faragha

Hatimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Haki zote Zimeifadhiwa.